MBUNGE jimbo la Kilolo, Profesa Peter
Msolla ametoa Sh 150,000 kama mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Ndengisivili, wilayani
Kilolo.
Wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi
wa kanisa hilo, waumini zaidi ya 120 wa usharika huo wanaabudu katika jengo la
muda lililojengwa kwa tope huku likiwa limeezekwa kwa nyasi.
Profesa Msolla alitoa mchango huo
hivikaribuni alipofanya ziara ya kijimbo katika kijiji hicho kwa lengo la
kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya
CCM kwa kipindi cha mwaka uliopita.
Mchango huo kwa mujibu wa Mchungaji wa
Usharika huo, Damas Chavalla utasaidia kununua sehemu bati ziatakazotumika
kuuzekea kanisa hilo.
Mchungaji Savalla alisema ujenzi wa
kanisa hilo unaendelea kwa nguvu za waumini, wadau na KKKT Dayosisi ya Iringa.
“Mei 30 Baba Askofu Mdegella
atatutembelea ili aone maendeleo ya ujenzi huu; katika ziara yake hiyo
ataitumia kuhamasisha waumini na wadau wengine kutuchangia zaidi,” alisema.
Alisema ujenzi wa kanisa hilo
litakalokuwa la kudumu ulianza Desemba mwaka jana na unatarajia kukamilika
wakati wowote mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema kukamilika kwa kanisa hilo
kutaleta furaha kwa waumini wake kwa kuzingatia kwamba; “tunapata kero kubwa
wakati wa masika, jengo tunalotumia sasa ni la nyasi, wakati wa kipindi hicho
huwa linavuja sana na kuvuruga utaratibu wa Ibada.”
Alisema usharika pia unahitaji usafiri
utakaowawezesha kutoa huduma ya kutembelea vitongoji vya kijiji hicho na kurahisisha
ushiriki wa mikutano ya kijimbo.
Kijiji cha Ndengisivili kipo zaidi ya
kilomita 70 kutoka mjini Iringa yaliko makao makuu ya KKKT Dayosisi ya Iringa.
No comments:
Post a Comment