MSANII mahiri wa komedi ambaye pia ni Mwimbaji wa Injili,
Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ amenaswa akichati kwenye simu wakati viongozi wa dini
wakishusha maombi mazito.
Tukio hilo lililowachefua baadhi ya waumini lilitokea hivi
karibuni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Saba Saba, mjini Moro ambapo Masanja
aliyekuwa meza kuu, wakati wenzake wakiongoza sala ya kufungua kongamano hilo,
yeye alikuwa bize na simu.
Kitendo hicho kilidumu kwa dakika kadhaa kisha staa huyo ambaye
pia ana ndoto ya kuwa mchungaji mkubwa nchini, akajiunga na wachungaji wengine
waliokuwa meza kuu kuendelea na sala.
No comments:
Post a Comment