Showing posts with label SHE PONDA. Show all posts
Showing posts with label SHE PONDA. Show all posts

Monday, August 19, 2013

HAYA NDIO MASHTAKA MATATU ALIYOSOMEWA SHEHE PONDA.


Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi  kutenda kosa.  
  
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi  chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...

SHEHE PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI,,HELKOPTA YATUMIKA KUMSAFIRISHA KUTOKA DAR HADI MOROGORO



Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda muda huu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro. 

Sheikh Ponda amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali akisindikizwa na msafara wa magari yaliyokuwa na polisi. 
  
Ponda amesafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam mpaka mkoani Morogogro kwa usafiri wa helkopta iliyotua katika viwanja vya Gymkhana. 

Sunday, August 18, 2013

KUTEKWA KWA PONDA NI HARAKATI ZA SERIKALI KUWAPENDELEA WAKRISTO,,NI UJUMBE UNAOSOMEKA KATIKA VIPEPERUSHI WANAVYOSAMBAZA WAISILAMU



SAKATA la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, limeendelea kuwa gumzo katika maeneo mbalimbali, huku matamko makali yakitolewa dhidi ya Serikali.

Sakata hilo limeonekana kutikisa na kutawala vyombo vya habari, baada ya kiongozi huyo wa dini kudaiwa kupigwa risasi, kusomewa mashtaka kitandani na baadaye kupelekwa gerezani chini ya ulinzi mkali akitolewa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).

Suala hilo limeibua hisia nyingine baada ya masheikh jijini Dar es Salaam, kutoa tamko lenye mwelekeo wa kupinga udhalilishwaji wa kiongozi huyo na kuionya Serikali juu ya mwenendo huo.

Thursday, August 15, 2013

SHEHE PONDA ASOMEWA MASHTAKA YA UCHOCHEZI AKIWA HOSPITALINI.


Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda amesomewa mashitaka ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa wodini MOI anapoendelea kupata matibabu.

Sheikh Ponda arijeruhiwa Jumamosi iliyopita akiwa katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani Morogoro.
  
Baada ya kujeruhiwa Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) aliposomewa mashitaka. 

Kesi yake itaendelea pindi atakapopata nafuu


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...