STAA wa Filamu ya
Foolish Age, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hivi sasa anakesha akiomba ili
mambo yaende vizuri katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii
mwenzake, Steven Kanumba, Ijumaa lina maelezo yake ya kutosha.
Lulu amemwambia paparazi wetu kuwa alishaanza kuyasahau matatizo hayo lakini hataweza kupingana na amri ya mahakama iliyopanga kuanza kusikiliza kesi hiyo kuanzia Februari 17, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar.
“Lazima kesi iendelee na sheria ichukue mkondo wake, pamoja na kwamba nimekaa uraiani kwa kipindi kirefu na kuanza kusahau mambo hayo,” alisema Lulu.