Makubwa! Kwa mara kwanza mama mzazi wa
mwigizaji mkongwe Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye hakupenda jina
lichorwe gazetini ameibuka na kumfumua staa wa filamu ‘mbia’ wa mwanaye,
Vincent Kigosi ‘Ray’, Risasi Jumamosi lina cha kushika.
Akizungumza na mapaparazi wetu katika mahojiano maalum
nyumbani kwake, Ubungo External, Dar, wiki hii, mama Johari alifunguka kuwa
hamjui wala hajawahi kumuona Ray ambaye ni mkurugenzi mwenza wa Johari. Ndiyo
wamiliki wa kampuni ya kufyatua filamu ya RJ Productions.