Showing posts with label CHADEMA. Show all posts
Showing posts with label CHADEMA. Show all posts

Saturday, February 22, 2014

KUMEKUCHA KALENGA,KAMPENI ZA KUWANIA UBINGE WA JIMBO HILO KUZINDULIWA LEO KWA UPANDE WA CHADEMA,HUKU CCM WAKIJIPANGA KUZINDUA KESHO.


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa leo Jumamosi atazindua kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa katika kijiji cha Kalenga.

Kwa upande wao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitanzaa kampeni zake keshokutwa Jumapili katika kijiji cha Mseke wakati kikiendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hizo.

Saturday, August 31, 2013

BAADHI YA MAONI YA CHADEMA KUHUSU KATIBA MPYA.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeeleza kuiunga mkono rasimu hiyo kwa asilimia 80 kulingana na maoni ya watu milioni 3.4 waliokusanya.Hata hivyo, CHADEMA imeainisha hoja 11 ambazo wananchi wamependekeza ziongezwe katika rasimu hiyo ya Katiba mpya.Akizungumza na waaandishi wa habari jana makao makuu ya chama hicho, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema mrejesho huo umepatikana baada ya kuwazungukia wanachama wao na Watanzania wengine kwa wiki mbili.Dk. Slaa alisema maoni hayo yamekusanywa kupitia kanda 10 za chama hicho na Watanzania waishio nje ya nchi kwa njia ya kisayansi huku yakiwa na vithibitisho tofauti na vyama vingine vya kisiasa.

Monday, August 19, 2013

SERIKALI YAENDELEZA UBABE HUKO MWANZA,,WAANDAMANAJI WAKUTANA NA DHAHAMA YA MABOMU KUTOKA KWA POLISI.



MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuwa  yakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela  pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha na yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa MwanzaErnest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...