Inakuaje
pale wanafunzi wa form six ambao wanatarajiwa kujiunga na chuo kikuu wanafeli
wote nchi nzima na kushindwa kujiunga na chuo kikuu?.Kwa mara ya kwanza katika
historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani
wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye
atafuzu kuingia chuo kikuu.
Chuo
kikuu cha Liberia kwa mwaka 2013/2014 hakitakuwa na mwanafunzi hata mmoja kwa
ajili ya kozi yoyote ile kutokana na wanafunzi hao kufeli. Waziri wa elimu wa
Liberia anasema wanafunzi wameshindwa kufaulu mtihani huo kutokana na lugha
walioitumia ya kiingereza. Wanafunzi hao hawakuwa na uelewa mzuri wa lugha ya
kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Hata
hivyo wanafunzi wengi hawana imani na matokeo hayo na waziri wa elimu anajaribu
kuongea na chuo kikuu cha Liberia kuona jinsi watakavyofanya.
No comments:
Post a Comment