Yeyote
ambae damu yake ipo sana kwenye muziki wa bongofleva ni lazima atakua anafahamu
kuhusu ugomvi wa muda mrefu, kutoelewana kwa Chidi Benz na Ney wa Mitego, ishu
ambayo ilihusishwa hata kwenye nyimbo zao.
Shuhuda
mkuu wa tukio lenyewe ni msanii Madee ambae naanza kwa kumkariri anasema ‘hizi
ndio faida za Serengeti Fiesta, kujuana na kukutana na watu wengi, hiki ni kitu
ambacho nilikipanga mimi… watu wanafikiria tu sisi tunakwenda kule kufanya muziki,
mbali na pesa tunazolipwa vizuri sasa hivi kwenye Fiesta, kuna faida nyingine
pia, niliposikia Chidi Benz yupo kwenye Fiesta nilijipanga lazima nifanye hivi
manake Chidi na Ney wote nawajua, nimekaa nao’
Kwenye
sentensi ya pili, Madee anasema ‘niligundua Chidi ni mwepesi kukasirika, kuna
wakati kwenye basi la Wasanii kulitokea kama purukushani kuhusu hawa wawili so
nikasubiri tu time nzuri ifike nifanye yangu’
‘Nilipoona
Chidi katulia nikamfata, nikamchukua alafu bila kumwambia kitu nikampeleka
mpaka alipokuwepo Ney wa Mitego, nikamwambia haya…. simama pale nikupige picha,
wakati huo sijasema chochote kuhusu ugomvi na Shilole alikua ndio kasimama na
Ney, nikawapiga wakiwa watatu alafu badae nikamwambia Shilole aondoke wakabaki
wawili, yani Ney na Chidi’ – Madee
Madee
anakwambia baada ya kupiga picha hazikuongelewa stori zozote za ugomvi wa Chidi
na Ney, kwanza zilipigwa stori za mtaani tu… za ujana alafu kitu kikaitika
manake Ney wa Mitego na Chidi Benz wote walikua na furaha na walikua
wanachangia mada kwa pamoja, yani kama washkaji….
Hii
ishu ilitokea wakati wa show ya Serengeti Fiesta 2013 Singida 89.7 ambapo badae
walikwenda Club ambako huko sasa ndio waliongea kwa kirefu, kikubwa alichokua
anaongea Chidi ni kuhusu Ney kumuimba vibaya kwenye nyimbo zake lakini Ney
aliweka wazi kwamba nia yake sio mbaya na wala anachokitaka sio ugomvi bali ni
aina ya muziki wake, kwa mujibu wamaelezo ya Madee.
Kingine
anachosema Madee ni ‘Ney ndio aina ya muziki wake, hawezi kung’aa mpaka amtaje
mtu kwenye nyimbo zake na hiyo ni bishara yake, lakini anavyofanya hivyo sio
kwamba anataka ugomvi, ni mtu muelewa na wala sio mtu wa aina hiyo ya
ugomviugomvi, baada ya kuwapatanisha wakashikana mikono, tukawaambia
wabadilishane namba za simu alafu bata likaendelea… so sasa hivi kila kitu ni
fresh’
Kama
ulikua hujui, Ney wa Mitego alishawahi kuwa na ugomvi na Madee zaidi ya miaka
10 iliyopita ambapo mama mzazi wa Madee aliwahi kupigwa chupa ya uso mpaka leo
anayo alama usoni wakati akiamulia ugomvi wa Madee na Ney wa Mitego ambae
alimfata Madee nyumbani kwao akiwa na wenzake wakitaka kumpiga.
No comments:
Post a Comment