Hit maker wa muziki gani,nasema nao,na salamu zao, Ney wa
Mitego, ameweka wazi kuwa ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili
ya kuendesha mipango ya msiba wake, "#kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo
kwa ajili ya kuvuna pesa".
Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe mfupi kwenye
simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba kwenye single yake mpya
ya 'Salaam zao' .
Ujumbe huo wa vitisho ambao umepokelewa na msanii
huyo umekuja mara baada ya msanii huyo kuachia single yake hiyo ambapo moja ya
mashahiri ni juu ya hela za rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii
Ngwear pamoja na Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.
Akizungumza na jarida la Maisha, mara baada ya
kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea
ujumbe wa vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.
Alisema kuwa amepokea ujumbe mbalimbali ambazo zipo
zinazowataja wahusika moja kwa moja wale waliohusika kula rambirambi, huku
wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.
"Mimi hata ikitokea
nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa kuweka kamati ya mazishi yangu
kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi hizo
kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa
Mitego.
Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata
kama ataendelea kupokea vitisho.
No comments:
Post a Comment