Baadhi
ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka wilaya
ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya
magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA
LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa
Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya
ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa
Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya
ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo.
===============
Mnamo
tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya
Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara
wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano
Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na
tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa
nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na
vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya
barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.
Katika
ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1.
STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2.
STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu
Tawala [M] Dodoma.
3.
SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4.
DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma.
5.
T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6.
STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao
tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika
Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa
kurudi nyumbani.
Majeruhi
waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1.
JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa,
Mkazi wa Kusini Unguja.
2.
CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3.
DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa
Mailimbili.
4.
AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’
Manispaa ya Dodoma.
Majeruhi
waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1.
JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa
Area C Manispaa ya Dodoma
2.
RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa
Ipagala Manispaa ya Dodoma
3.
JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa
Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4.
ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara
hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa
makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara
yanayoweza kuepukika.(soma zaidi hapahttp://talkbongo.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment