RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi
za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu
Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali, ambapo wapo waliohamishwa,
wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.
Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
- Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia.
- Joyce
Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,
Biashara na Masoko.
- Jumanne
Sagini amekuwa Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali
alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.
- Dk Servacius
Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, awali alikuwa
Naibu Katibu Wizara ya
Fedha.
- Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali
alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.
- Alphayo
Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI.
- Dk Shaaban
Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, awali alikuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
- Dk Uledi
Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara
na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
- Profesa Sifuni
Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
- Charles
Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.
- Anna
Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii
Jinsia na Watoto, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo.
- Sihaba
Nkinga amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara hiyo.
- Sophia
Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Balozi Sefue aliongeza kwamba:
- Katibu
Mkuu aliyepewa uhamisho ni Peniel Lyimo ambaye
anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu kwenye “Presidential’s Delivery
Bureau” kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza
Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu.
Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-
- Sethi
Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
- Kijakazi
Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto
- Injinia Omari Chambo aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi
Katibu anayestaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye sasa amestaafu kwa hiari.
Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao. Aliiwataja Naibu Makatibu Wakuu wapya walioteuliwa kuwa ni:-
- Angelina Madete amekuwa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
- Regina
Kikuli amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
- Zuberi
Sumataba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI, anayeshughulikia suala la elimu katika ngazi za
Serikali za Mitaa
- Edwin
Kiliba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI
- Deodatus
Mtasiwa amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la afya upande
wa Serikali za Mitaa.
- Dk Yamungu
Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika
- Profesa Adolf
Mkenda amekuwa Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia sera
- Dorothy
Mwanyika amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni
- Rose
Shelukindo amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa
- Dk Selassie
Mayunga amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi
- Monica
Mwamunyange amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi
- Consolata
Mgimba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
- Profesa Elisante
ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
- Armantius
Msole amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano
wa Afrika Mashariki
Balozi Sefue aliwataja Naibu Makatibu Wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni:-
- John
Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo
- Selestine
Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii,
anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
- Injinia Ngosi Mwihava anahamia
Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais
- Maria
Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
- Nuru
Milao anahamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment