Monday, August 19, 2013

HAYA NDIO MASHTAKA MATATU ALIYOSOMEWA SHEHE PONDA.


Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi  kutenda kosa.  
  
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi  chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...



Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard  Kongola amedai kuwa shekh Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro.


Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua kupeleka jeshi  Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu. 



No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...