MBALI ya jitihada mbalimbali
zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari kuwa unywaji wa
pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, ‘janki’ Geoffrey Mlelwa (26), mkazi wa
Ipogolo mjini hapa, amejikuta akiyakatisha maisha yake kwa kudaiwa kugida pombe
kupindukia.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo kijana huyo
alikuwa katika Soko Kuu la Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake wakipiga ulabu
kwa staili ya kuchanganya (kuchoma sindano) ndipo Geoffrey alipopitiliza na
kusababisha apoteze uhai.
No comments:
Post a Comment