Jeshi la Polisi Mkoa
wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New
Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Wanaoshikiliwa ni Kevin
Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John
Joseph(aliye kaa katikati)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime
kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa
Basi la New Force
lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa
muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma
linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na bhangi kiasi cha Kilogramu
133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value).
Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stendi Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stendi Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bhangi katika mabegi baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam.
Watu hao walifahamika kwa majina ya:-
1.
CALVIN S/O PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila
Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es
Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito
51kgs.
2.
JOHN S/O JOSEPH, Miaka 31, kabila Msukuma,
mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mabegi mawili
ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
3.
JOSEPH S/O CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila
Msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga. alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya
bhangi yenye uzito 36.5kgs
Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za
raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia
kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya
nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia
manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi.
No comments:
Post a Comment