katika list ya wasanii wa hiphop wenye mkwanja
mrefu 2014 iliyotolewa na Forbes mtu mzima Diddy ameshika nafasi ya kwanza.
Puff Daddy ameshika
nafasi hiyo ya juu katika wasanii wa hiphop bora watano wenye mkwanja mrefu
katika list ya forbes iliyoachiwa mapema siku ya jana (April 6). Diddy
ambae pia anajulikana kama Sean "Diddy" Combs ana thamani ya dolla
milioni 700, kutokana na kilichoandikwa na gazeti hilo.
Revolt Tv ambayo aliizindua miezi michache
iliyopita inamuingizia mkate mkubwa kiasi kwamba kwa siku moja inaweza kumfanya
kuwa msanii bilionea wa kwanza wa hiphop, story hiyo iliendelea kusema.
Dr Dre amekamata
nafasi ya 2 katika list hiyo, Andre Young ambae ni Rapper na Producer mkwanja
mwingi aliotakwa kuwa nao ambao ni dolla milioni 550 zinatokana na mzigo wa
headphones "Beats by Dre" kampuni ya headphone ambayo alianzisha na
Jimmy Lovin 2008
Jay Z ametua katika nafasi ya 3. dili lake na
Rocawear pamoja na Live Nation imemuingizia dolla milioni 150, iliyomsaidia
kuongezea na kufika kukusanya dola milioni 520
Brian "Birdman" Williams ambae
pia anajulikana kama Baby, ameingia katika nafasi ya 4 ya list ya Forbes,
asilimia zake 50 kutoka Cash Money Records inamuingizia zaidi katika mkwanja
wake ambao ni dola milioni 160
Na wa tano ni Curtis Jackson
a.k.a 50 Cent ambae utajiri wake mkubwa unatokana na maji yake ambayo
ameyaita Vitamin Water ambayo yamemsababishia kupata kile kilichoripotiwa kuwa
ni dola milioni 100
No comments:
Post a Comment