WAJUMBE
wa Bunge Maalumu, wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema
hawatarudi bungeni na badala yake kuanzia kesho wataanza mikutano ya hadhara
nchi nzima kuwaeleza wananchi juu ya hila za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
washirika wake kutaka kuhodhi mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.
UKAWA
wamesema katika mikutano hiyo watazisambaza ‘CD’ zinazomuonesha Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akiwa katika
Kanisa la Methodist, mkoani Dodoma akiwaeleza waumini wakatae muundo wa
serikali tatu.
Walisema
kwenye CD hizo, Lukuvi, anaonekana akiwaambia wananchi iwapo wataridhia muundo
wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi na Zanzibar itaingia katika utawala wa
Kiislamu.
Juzi
wajumbe wa UKAWA walisusia kikao cha Bunge Maalumu kwa madai ya kuchoshwa
kusikiliza matusi, ubaguzi na kauli za chuki zinazotolewa na wajumbe kutoka CCM
bila viongozi wakubwa kukemea.
Jana
wakizungumza na waandishi wa habari, viongozi wa UKAWA walisema hawatarejea
bungeni mpaka watakapoketi
Jana
wakizungumza na waandishi wa habari, viongozi wa UKAWA walisema hawatarejea
bungeni mpaka watakapoketi kwenye vikao vya maridhiano ambavyo pia watakwenda
na masharti yao mojawapo ni rasimu ya Tume ya Warioba ndiyo iwe msingi wa
majadiliano.
Masharti
mengine ni kukaa kwenye meza ya maridhiano na viongozi wa serikali na CCM,
kusiwepo matusi, ubaguzi na kauli za chuki.
Mmoja wa
viongozi wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa watazunguka nchi nzima
kuwaeleza wananchi kilichotokea bungeni na namna CCM wanavyopenyeza rasimu yao
kwa mlango wa nyuma.
“Sisi tupo
tayari kwa mazungumzo kama tulivyoombwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel
Sitta, lakini hatutakubali kubeba matakwa ya CCM, tunataka tujadili rasimu ya
Tume ya Jaji Warioba ambayo ilikwenda kuwahoji wananchi,” alisema.
Profesa
Lipumba, alisema wameamua kususa vikao vya Bunge kwa sababu hawako tayari
kushiriki kupitisha masuala yenye masilahi ya CCM yaliyopelekwa bungeni kwa
mlango wa nyuma.
Alisema
walitegemea wajumbe wangejikita kujadili rasimu iliyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kwa hoja lakini badala yake wameshuhudia matusi, ubaguzi,
kauli za chuki ambazo zinachangia zaidi kuligawa taifa.
Lipumba
alisema rasimu iliyopo mezani inataja serikali tatu hivyo kama wajumbe wa CCM
wanataka kujadili serikali mbili, lazima Bunge livunjwe na iundwe tume nyingine
itakayotoa rasimu ya serikali mbili.
“Wenzetu
wanatushangaza sana yaani walivyokuwa wakijadili rasimu ile kama imetolewa na
wapinzani, hii ni rasimu iliyotolewa na tume iliyoundwa na rais, sasa kama
wenzetu hawaamini sisi tunakwenda kuwaeleza wananchi CCM isivyotaka kuandika
Katiba yenye masilahi ya wananchi,” alisema.
Lipumba
pia alisema Chama cha Wananchi (CUF), kitaangalia hatua za kisheria za
kumchukulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
William Lukuvi, alivyokihusisha chama hicho na taasisi ya kidini ya UAMSHO.
Alisema si
kweli kwamba CUF imekuwa ikishirikiana na taasisi hiyo ambayo mara kadhaa
imekuwa ikihusishwa na mihadhara ya kidini yenye vurugu visiwani Zanzibar.
Naye James
Mbatia, alisema maridhiano ndiyo yatakayosaidia mchakato wa Katiba kusonga
mbele lakini kwa hali inavyoonekana CCM hawana dhamira ya kuandika Katiba yenye
kujali masilahi ya wananchi.
Alisema
wiki iliyopita TCD iliitisha mkutano wenye lengo la kutafuta maridhiano lakini
CCM walituma wawakilishi wasio na nyadhifa za juu kama zilivyofanya pande
nyingine.
Naye
Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, alisema wameamua kususa vikao vya Bunge
kwakuwa wajumbe wengi kutoka CCM wameacha kujadili rasimu iliyowasilishwa na
Tume ya Warioba ambayo ndiyo msingi wa majadiliano yao.
Alisema
Tume ya Warioba iliwekwa kisheria na ilifanya kazi ya kuwahoji watu pamoja na
kutumia nyaraka mbalimbali hadi kufikia kutoa rasimu isiyotakiwa na wajumbe wa
CCM walioanza kujadili rasimu waliyopewa na chama chao.
“Kususia
vikao vya Bunge ni miongoni mwa hatua za kutafuta haki, kuendelea kushiriki
vikao hivi ni kuhalalisha na kubariki udhalimu wa CCM ambayo imeamua kukwamisha
Katiba mpya.
“Matusi,
ubaguzi, chuki haviwezi kutusaidia kupata Katiba mpya, UKAWA hatuko tayari
kuendelea kushiriki majadiliano yenye mambo hayo….tunakwenda kwa wananchi
kuwaeleza kile kinachofanywa na wajumbe humu bungeni,” alisema.
Mbowe
alisema si lazima Rais Jakaya Kikwete aondoke madarakani wakati Katiba mpya
imepatikana bali mchakato huo unaweza kuendelezwa na rais mwingine lakini
katika mazingira yanayokubalika na watu wote.
Posho
Hata hivyo
wajumbe wa Katiba, walikuwa wakipigana vijembe kuwa UKAWA wameamua kususa vikao
vya Bunge baada ya kulipwa posho ya vikao mpaka Aprili 22 mwaka huu.
Said
Nkumba, alisema UKAWA ni wanafiki kwakuwa wamesusia vikao hivyo baada ya
kulipwa fedha hizo na kama wasingelipwa wasingethubu kulikimbia Bunge.
Livingstone
Lusinde, alisema UKAWA, hawana ujasiri wa kutetea masilahi ya umma bali wapo
kwa ajili ya kuangalia masilahi binafsi ndiyo maana waliondoka bungeni baada ya
kusikia wamelipwa fedha mpaka Aprili 22.
Naye Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu, Nchemba, alisema jana waliwasiliana na
benki kuona kama zilikuwa zimefanya malipo kwa wajumbe hao wazuie fedha hizo
ili kuwadhibiti wajumbe wa UKAWA ambao wanachukua fedha bila kufanya kazi
Hata hivyo
kauli hiyo ilionekana kupinga na Katibu wa Bunge, Yahya Khamis, aliyesema fedha
hizo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti za wajumbe.
Khamis,
alisema kuanzia Aprili 22, ndiyo watajua kama wajumbe wa UKAWA, hawatahudhuria
vikao vya Bunge hawataingiziwa fedha za kujikimu na ile ya vikao.
Kwa siku
moja wajumbe hao wanalilipwa sh 300,000 ambapo sh 230,000 ni posho za kujikimu,
sh 70,000 posho ya vikao.
Makatibu
Wakuu UKAWA watoa kauli
Makatibu
wakuu wa UKAWA wamesema wabunge wao hawatarejea bungeni badala yake watazunguka
nchi nzima kuelezea namna serikali ya CCM isivyotaka wananachi wapate katiba
wanayoitaka.
Mbali ya
msimamo huo, pia wameeleza mbele ya waandishi wa habari kuwa kuwa Rais Jakaya
Kikwete alipopata fursa ya kulihutubia Taifa wakati wa kulizindua bunge, alianzisha
vita ya kisiasa na kuigawa nchi vipande kutokana na vitisho alivyovitoa kama
mkuu wa nchi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, alisema
wao kama makatibu wakuu wanaunga mkono wabunge wao kutoka nje na kukiita
kitendo hicho kuwa ni cha kishujaa na uzalendo wa kukataa kuburuzwa.
Alisema
hakuna chama kinachotaka Katiba Mpya kwa dhamira ya kuvunja muungano kama
wanavyodai CCM, badala yake wanataka katiba ya maridhiano yanayoongozwa na
uamuzi wa wananachi.
“Haya ni
mapambano na vita inayohitaji kuunganisha nguvu zote kwa kuwa hili ni
jambo kubwa kwa mustakabali wa taifa na tunapoona watu wanafanya masikhara kwa
ajili ya masilahi na misimamo ya vyama vyao, hatuwezi kukubali,” alisema Dk.
Slaa.
Aliongeza
kuwa kuna hatari ya mfumo uliozaa katiba inayotumika sasa kurejeshwa katika
mfumo mzima wa upatikanaji wa katiba mpya na kwamba kama vyama vya siasa
walionya hali hiyo mapema kwa ajili ya kulinda umoja wa kitaifa.
“Tulikuwa
tayari kuridhiana kuanzia mwanzo lakini wenzetu hawataki maridhiano zaidi ya
misimamo yao inayolindwa na wingi wao ndani ya bunge, sasa sisi tuna watu nje
ya bunge na kama wanasema kuwepo kwa serikali tatu jeshi litapindua nchi huo ni uongo, kama mapinduzi
yangefanyika sasa kwa kuwa wamewadhulumu hao wanajeshi hata hela zao za
Operesheni Tokomeza,” aliongeza Dk. Slaa.
Dhana ya
Vitisho
Kaimu
Katibu Mkuu wa CUF, Shaweji Mketo, alisema ni jambo la kusikitisha kuona
serikali inatumia vitisho kwa wananchi wakati walibariki mchakato mzima wa
kukusanya na kuandika maoni ya wananchi ya kupatikana katiba mpya
Mketo
alisema kitendo cha wabunge wao kutoka nje kilitosha kulivunja bunge kwani
rasimu haisemi mjadala wa serikali mbili.
UKAWA
haitarudia makosa
Katibu
Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, Mosena Nyambabe, alisema kulikuwa na makosa
mengi wakati vyama vya siasa viliporidhia kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi
mwaka 1992 bila kupata katiba mpya.
Alisema
hoja zinazotolewa kuwa wapinzani hawataki katiba mpya zinapotoshwa makusudi,
kwa kuwa madai ya vyama vya upinzani kuhusu katiba ya wananachi yalianza miaka
ya 1960.
No comments:
Post a Comment