BAADA ya hivi
karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki na filamu Bongo, Snura
Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga ambapo hivi karibuni alipata
msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata ajali.
Akizungumza kwa
huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu yake huyo
alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi kufikia utu uzima.
“Ukweli nimeumia
sana na mwaka huu umekuwa ni wa majanga kwangu kwani babu yangu huyo nilikuwa
namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea mpaka nikafikia umri huu
nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya yuko hoi hospitali, utumbo
ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni, nimechanganyikiwa,” alisema Snura.
No comments:
Post a Comment