Emmanuel
Okwi ambae ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyesajiliwa na klabu ya
Yanga, ameruhusiwa rasmi kikiwa ni kibali kutoka shirikisho la soka
duniani (FIFA) kushiriki kuichezea timu yake ya sasa ambayo ni Yanga.
Okwi ambaye alikuwa amesimamishwa
kutokana suala la mgogoro mauzo yake uliokuwa ukizihusisha timu zake za zamani
Simba SC ya Tanzania na Etoile Du Sahel ya Tunisia, sasa ameruhusiwa kuitumikia
Yanga huku FIFA ikiendelea kufuatilia kiundani kuhusu deni la Simba la dola
300,000 wanaloidai Etoile.
Fedha hiyo ilikuwa ya
uhamisho wa mchezaji huyu kutoka Simba kwenda Tunisia takribani miaka miwili
iliyopita ambapo baada ya kupata greenlight, Okwi sasa ataweza kuitumikia Yanga
katika michuano ya ligi kuu na kombe la klabu bingwa ya Afrika.
No comments:
Post a Comment