Monday, August 19, 2013

ZITOO KABWE AKANUSHA UVUMI ULIOENEA JUU YA KUJITENGA KWAKE NA HARAKATI ZA CHADEMA.


Kuna taarifa zimeenea kwenye mitandao  kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara CHADEMA, Zitto ataanza safari ya kuimarisha chama katika mikoa 5 hapa nchini na kwamba inatokana na yeye 'kujitenga' na ziara inayoendelea hivi sasa ya Mabaraza Huru ya Katiba Mpya, kukiwa na timu mbili, chini ya viongozi wakuu wa kitaifa, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, ambapo kila timu inatumia usafiri wa chopper!

Wana CHADEMA wawe makini na upotoshaji au hila za kuwaondoa kwenye focus ya suala la Katiba Mpya, hasa ambapo kwa sasa chama kinakusanya maoni ya wanachama na wapenzi wake juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwenye mikutano ya hadhara inayoendelea nchi nzima.


Maandalizi yaliyopo kwa ajili ya ziara ya Naibu Katibu Mkuu, si kwa ajili ya mikoa 5 kama ilivyopotoshwa, bali ni mikoa 3 ambayo ndiyo inayounda Kanda ya Magharibi, ambapo yeye akiwa kiongozi mwandamizi wa chama kutoka kanda hiyo, pia kama mbunge wa eneo husika, pamoja na viongozi wengine wa chama katika mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora, anawajibika kuhakikisha kanda hiyo inatimiza majukumu yake kwa kadri ya malengo na maelekezo ya chama, yaliyoamuriwa kwenye vikao.

Ziara ya Naibu Katibu Mkuu, kama ilivyo ziara za kichama za viongozi wengine huwa zinatolewa taarifa rasmi. Wakati ukifika, baada ya kuwa taratibu zote, ikiwemo kupitishwa katika vikao na 'modes of operandi' kuwekwa, umma utajulishwa na kupewa taarifa ya ziara.

Hapa chini ni response ya Naibu Katibu Mkuu Zitto juu ya taarifa hizo zenye upotoshaji na bila shaka zikilenga kuwaondoa wana CHADEMA kujikita kujadili masuala ya msingi ambayo chama chao, kwa niaba ya Watanzania, kinapaswa kuyasimamia katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya mstakabali wa nchi yetu na jamii nzima ya Watanzania kwa ujumla.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Moja, sijajitenga na ziara ya chopa. Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, kamati hii inasimamia mahesabu ya Serikali. Ziara inafanyika kipindi cha kamati za Bunge na hivyo sikuweza kushiriki kwani ni hatari mno kuacha PAC chini ya wabunge wa CCM peke yake. Leo kamati inahoji Wizara ya Elimu yenye madudu kibao, Hazina yenye kukusanya mapato yote ya Serikali na ratiba nzima nitawasilisha hapa. Haya yote uongozi wa chama unajua. Ni mgawanyo tu wa majukumu. Hata hivyo nimeshiriki kuandaa mikutano katika mkoa wa Kigoma na gharama zote za maandalizi nimetoa mimi. Hata gari anayotumia mwenyekiti huko Kigoma ni gari yangu. Kusema nimesusa ni uzushi sana wenye lengo la kuleta mgogoro kwenye chama.

Pili, mimi ni mbunge kutoka Kanda ya Magharibi. Kila kanda imepewa wajibu wa kujiimarisha kichama. Nimekuwa nilifanya hivi toka kanda zimeundwa. Kuanzia mkutano wa mwanzo nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kuhakikisha kwamba kanda ya magharibi inakuwa imara kichama. Nimefanya ziara kadhaa mkoa wa Kigoma na mkoa wa Tabora. Hivi sasa kanda zote zinapaswa kufanya uchaguzi wa ndani ya chama. Nimeamua kuanzi tarehe 20 Septemba (mara baada ya Bunge mkutano wa 12 kumalizika) kuanza ziara ya kanda ya magharibi kuchochea ujenzi wa chama kuanzia matawi ili tuweze kuendana na ratiba ya uchaguzi. Ziara hii itafuata taratibu zote za chama na sijaamua naifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa na katibu Mkuu.

Ninasikitika sana kwamba kumekuwa na tabia za kuchonganisha viongozi wa chama bila sababu kwenye mitandao ya intaneti. Kwa mtu anayeipenda chadema hawezi kufurahi mambo haya.

Mimi kama Zitto siwezi kufanya jambo lolote la kuathiri chama changu ambacho nimeshiriki kukijenga kwa kadiri ya uwezo wangu. Ninaomba pia watu wengine watumie muda zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagwa. Tunahitaji sana umoja na mshikamano wa dhati


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...