Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari hilo.
Mara baada ya dereva kugundua kuwa gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha na kuwaambia abiria wake kuwa gari linaungua.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni.
Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Wabunge waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu), Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar), Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo), Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini).
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
No comments:
Post a Comment