Thursday, August 15, 2013

MWIGULU NCHEMBA MATATANI.!!



Mmoja wa wahariri wa gazeti la mwananchi, Dismas Lyasa,ameomba kazi ya ukuu wa wilaya kwa Mwigulu Nchemba,taarifa ndani ya CCM na serikali zinasema, Mwigulu amevujisha taarifa za Lyasa kutaka kupewa nafasi hiyo kwa marafiki zake.

Pamoja na kuwa Mwigulu hana uwezo wa kutoa kaz ya nafas hiyo, isipokuwa ana ushawishi kwa rais na pinda ambae ndio wenye uwezo wa kutoa kazi nafasi hiyo.

Akiandika kwa Mwigulu, agosti 3 jumamosi mwaka huu,Lyassa ambae ni mhariri wa kijarida cha ''habari ndani ya habari'' katika gazeti lka Mwananchi ameomba,''....ningefurahi kupata fursa ya kuwa DC wa kilombero''

katika maombi yake Lyasa ameambatanisha cv na amemhakikishia Mwigulu kuwa yuko tayari kufanya kazi nae bega kwa bega na kwa staili yoyote .....
Lyasa anaandika,''nasikia kuna DC amerudishwa jeshini, na kwamba angefurahi kupata fursa ya kuwa mkuu wa wilaya huko.
Akiandika kwa njia ya kubembeleza,lyasa amesema, '' ninazo sifa za kuwa mkuu wa wilaya ya kilombero..
Lyasa anasema,naamin kama dc wa sasa ameshindwa kusaidia chochote,na ndio maana kiti cha udiwani Ifakara mjini kimeenda CHADEMA..anasema anayo mikakati mizito ya kuhakikisha kuwa CCM inakubalika kilombero,hivyo anaomba Mwigulu amsaidie kufanikisha mikakati yake hiyo. 
Lyasa pia anamtaadharisha Mwigulu kuwa, Dk Kitila Mkumbo,mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA ametangaza kugombea ubunge jimboni kwake (kwa mwigulu), mwaka 2015,lakin Lyasa akimpa moyo kuwa bado ana nguvu...
Source: mawio

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...