Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa
zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ” na wanyarwanda kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa
aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Madai hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa Rwanda.
No comments:
Post a Comment