Sunday, August 18, 2013

KATA KWA KATA KAMPENI KUIZIKA CCM NJOMBE.



Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Mkoani Njombe kimeanza mikutano yake ya kata kwa kata kwa lengo la kujenga chama ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wake.
Chama hicho ambacho kimeanza shughuli zake rasmi wiki iliyopita pia kupitia mikutano hiyo ina elimisha wananchi hao namna ya kuipata katiba mpya ambayo itazingatia matakwa na mahitaji yao na si matakwa ya wachache wenye nia ya kulihujumu Taifa.

Hatua hii imekuwa ni msumari mkali sana kwa chama cha Mapinduzi(CCM) ambao wamekuwa wakihaha huku na huko ili kuzuia watu wasihudhurie mikutano hiyo kwa kuhofia wananchi kukihama chama chao hivyo kuwahonga vijicent kidogo huku wengine wakitishiwa kufukuzwa kwenye vibanda vyao vya biashara.


Wakitoa kero zao wanawake wa kata hiyo kwa mgeni rasmi ambaye pia ni katibu CHADEMA wa wilaya ya Njombe Bwana Alatanga Nyagawa, wanawake hao walisema ni miaka mingi sasa wanahangaika na suala la maji japo swala hilo lilikuwa ni sehemu ya ahadi ya Mbunge wao Mh Deo Sanga ali maarufu kama JAH PEOPLE.


Wananchi hawa ambao pia wapo kwenye mchakato wa kupeleka mawazo yao kwenye mabaraza ya katiba wanausubiri kwa hamu ujio wa Mwenyekiti wa chama Mhe MBOWE akiambatana na Mhe John Mnyika pamoja na Mhe Tundu Lissu ambao wanatarajia kuhutubia mjini hapo tare 22/08 siku ya alhamis wiki ijao




Jana Jumamosi CHADEMA walikuwa katika kata ya UBENA katika mji wa makambako.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...