Makubwa! Kwa mara kwanza mama mzazi wa
mwigizaji mkongwe Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye hakupenda jina
lichorwe gazetini ameibuka na kumfumua staa wa filamu ‘mbia’ wa mwanaye,
Vincent Kigosi ‘Ray’, Risasi Jumamosi lina cha kushika.
Akizungumza na mapaparazi wetu katika mahojiano maalum
nyumbani kwake, Ubungo External, Dar, wiki hii, mama Johari alifunguka kuwa
hamjui wala hajawahi kumuona Ray ambaye ni mkurugenzi mwenza wa Johari. Ndiyo
wamiliki wa kampuni ya kufyatua filamu ya RJ Productions.
Mama Johari ambaye
pia ana makazi yake mkoani Shinyanga alisema alitua jijini Dar kwa matibabu ya
presha.
Baada ya kumjulia hali, mapaparazi wetu walitaka kujua
mama huyo anamzungumziaje Ray ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na
bintiye na kwamba ilishasemekana ni wapenzi.Ndipo mama huyo alipokuja juu akisema huyo Ray mwenyewe hamjui na hajawahi kumtia machoni zaidi ya kumsikisikia tu kama wengine.
“Mimi simjui huyo Ray na wala sijawahi kutambulishwa wala kuonana naye, kwanza siishi hapa nitamuonea wapi, nimekuja zangu kutibiwa tu kutokana na matatizo yangu ya presha na kisukari
“Kwanza mwanangu
hana muda wa kukaa na kumuumizia kichwa huyo Ray kwani yeye ni baba yake?
“Hata siku moja (Johari) hawezi kuishi kwa kumtegemea yeye (Ray),” aliongeza mama huyo.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama huyo alisema kamwe hawezi kuumiza kichwa kuingilia mambo ya mwanaye, kwa kuhofia maradhi aliyonayo na kujitia matatizoni kwa mambo asiyoyajua undani wake.

No comments:
Post a Comment