MBUNGE wa Jimbo la
Kilolo, Profesa Peter Msolla ameendelea kuhamasisha michezo katika jimbo lake
hilo kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za vijana na
wanawake za vijiji mbalimbali.
Katika ziara yake
aliyofanya hivi karibuni katika vijiji vya Lulanzi, Kilolo, Kitowo, Lusinga, Ndengisivili na Kidabaga, Prpfesa
Msolla alitoa jezi, mipira na vifaa vingine vya michezo kwa timu za soka na
mpira wa pete zinazoundwa na wavulana na wasichana katika vijiji hivyo.
“Michezo hujenga
afya, michezo ni uhai; inatuepusha na tamaa zingine za dunia na hatari ya ulevi
wa kupindukia na ngono zembe, lakini michezo ni ajira ya uhakika,” alisema.
Alisema michezo hasa
wa soka umekuwa ukiwatajirisha vijana duniani kote na akataka vijana wa Kilolo
kuitumia fursa hiyo kujenga afya zao huku wakijua kwamba ni ajira inayolipa
kuliko ajira nyingi duniani.
“Wako wachezaji
wanalipwa zaidi ya Sh Milioni 300 kwa wiki; mnawasikia akina Messi, Ronaldo na
kwa Afrika tunao wengi tu kama akina Drogba, Yaya Tour, Etoo na wengine wengi,”
alisema.
Alisema vijana wa
Kilolo na wengine kutokana maeneo mbalimbali nchini wanaweza kufikia viwango
vya wachezaji hao kama wataweka dhamira.
“Hata timu zetu kubwa
za Yanga na Simba zinalipa vizuri, mnajua kwasababu mnasikia wachezaji
wanavyosalijiwa na mikataba yao minono wanayopata,” alisema.
Akiwa katika kijiji
cha Kidabaga, Profesa Msolla alipewa ombi la kusaidia ujenzi wa michezo na
akaahidi kwa kupitia mfuko wa jimbo kuangalia uwezekano wa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment