Hii ni vizuri kuifahamu wakati unasherehekea siku hii ya Valentine na
yule umpendaye ni vizuri kujua maana halisi ya hii Valentine Day ambayo
imeapishwa kufanyika kila mwaka February 14.
Neno
Valentine lilitokana na jina ‘Valentino’ huyu alikuwa Mtakatifu wa Kiroma
aliyeitwa Valentino,siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya wapendanao na
wengi wanaiita ‘Valentine Day’ ni maadhimisho ambayo hufanyika kila
mwaka.
Watu
wengi husherehekea siku hii kwa kuonyesha upendo,kuthaminiana pamoja na
kujaliana kati ya watu wenye mahusiano mbalimbali ya karibu japo mara nyingi
siku hii hutumiwa na walio kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Valentine
Day,asili ya Siku hii ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa
kwa ajili ya kuupenda Ukristo na Kihistoria Mtakatifu Valentino alitumika kama
kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia.
Mfalme
Claudia alimkamata na kumfunga,Mtakatifu Valentino aliteswa kwa ajili ya Imani
yake ya Kikristo na Kufa February 14 Kwa ajili ya msimamo,imani yake na
kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza February 14 kuwa siku ya
Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.Happy Valentine Day
No comments:
Post a Comment