Monday, August 12, 2013

PAMOJA NA KUTUHUMIWA KUGAWA PENZI GEST,NIMEPIMA NA SINA UKIMWI!!! KAULI YA ROSE NADAUKA


Mwanadada Rose Ndauka ambaye hivi karibuni aliingia katika skendo ya kimapenzi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayechipukia, ameamua kuwa mmoja wa wasanii wachache wa Sanaa ya Filamu nchini kuamua kuanika wazi majibu ya vipimovyake vya gonjwa hatari la ukimwi nchini.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmmoja wa kijamii, Rose aliweka majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa wiki kadhaa zilizopita katika hospitali ya TMJ iliyopo jijini Dar es salaam, vikionesha kuwa mwanadada huyo yu SALAMA kabisa na safi kiafya ama HIV NEGATIVE kwa mujibu wa vipimo hivyo.

Katika picha hiyo Rose ndauka aliandika anamshukuru Mungu sana kwa majibu hayo.


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...