Thursday, August 1, 2013

NINA MAADUI WAKUU WAWILI, 1-DR SLAA NA WA PILINI SHETANI-KAULI YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM MH MWIGULU NCHEMBA.


GAZETI LA MAWIO

Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba amesema anao maadui wawili wakuu hapa nchini.

Akizungumza na gazeti la MAWIO Mwigulu amewataja maadui hao wawili kwamba adui wa kwanza ni Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa na adui wa pili ni Shetani.

Gazeti lilimtafuta Dr Slaa kujibu madai hayo ya Mwigulu naye akasema haraka kauli hiyo anaichukulia kwa tahadhari kubwa.

Hata hivyo Dr Slaa alisema Mwigulu siyo saizi yake hivyo kamwe hawezi kujibizana naye.

Kiongozi huyo amesema anadhani tatizo la Mwigulu ni kutokwenda shule na kama amekwenda basi atakuwa amepita kama ng'ombe kwenye josho ambalo halina dawa.

Dr Slaa pia ameongeza kwa kusema kamwe hawezi kumuogopa binadamu mwenzake wakati anafahamu ameumbwa kwa udongo.'Mlinzi wa maisha yangu ni Mwenyezi Mungu na malaika wake.Mwigulu ni nani?'Alihoji Dr Slaa.

Kiongozi huyo amesisitiza kwa kusema anayefahamu dhamira yake ni Mwenyezi Mungu.''Yeye ndiye anayejua kile kilichoko moyoni mwangu.Mwigulu ni udongo tu kama mimi.Hana uwezo wa kuhukumu wala kuchukua maisha yangu.Lakini kauli yake hiyo naichukua kwa tahadhari kubwa''



No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...