Tuesday, August 6, 2013

KUNA VYAMA VINAENDESHWA KAMA SACCOS,KAULI YA MH. MWIGULU NCHEMBA-CCM

MH.MWIGULU NHEMBA
Mh.Mwigulu nchemba leo Tar.6/08/2013 amefanya mahojiano na mlimani tv ofisi ndogo za CCM-Lumumba. Mwandishi wa mlimani tv alikuwa na uhitaji wa kujua nini maoni ya Mh.Mwigulu nchemba(Naibu Katibu mkuu wa CCM Tanzania bara) kuhusu utendaji kazi wa msajili wa vyama vya siasa aliye staafu Mzee J.Tendwa.Mh. Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema “Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi za dhati kabisa kabisa,namshukuru sana Mzee wetu J.Tendwa kwa namna alivyotuongoza vyama vya siasa hadi kufikia hapa. Kimsingi mzee wetu ametulea,ametuvumilia sana na amekuwa na busara sana katika maamuzi yake.Naamini angeamua kushikilia sheria kuna vyama vya siasa leo hii visingekuwepo, yaani ingebaki CCM tu. 


Uongozi wa mzee wetu J.Tendwa haukuwa wa kiimla,ameongoza kwa kuzingatia demokrasia ya vyama vingi na amekuwa sehemu na kiungo kikubwa cha ujenzi wa demokrasia halisi ndani ya taifa letu.
 Nasema haya kwa sababu kunavyama vinaendeshwa kama SACCOS au NGO flani,havina demokrasia yoyote kama vinavyojipambanua.Kuna vyama ndani ya nchi yetu tangu Uongozi wa Rais Mstaafu Mwinyi,Rais Mkapa hadi Rais Kikwete havieleweki na havitabiliki ni lini vitafanya uchaguzi wa uongozi ndani ya vyama vyao. Yaani mwenyekiti ni yuleyule kuanzia chama kinaanzishwa enzi hizo hadi leo,Je hii ndio demokrasia?,Mzee J.Tendwa ametulea sana,na anastahili pongezi za dhati kabisa kabisa. 

MALALAMIKO YA VYAMA VYA UPINZANI KUHUSU UTENDAJI KAZI WA MZEE J.TENDWA
. 

Mh.Mwigulu Lameck Nchemba ,Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara alikuwa na haya ya kusema “Kwanza napenda kusema hakuna kazi ya binadamu isiyokuwa na mapungufu,vivyo hivyo kwenye utendaji kazi wa mzee wetu J.Tendwa yawezekana kunasehemu alikuwa na mapungufu yake lakini asilimia zaidi ya 90 amefanya kazi yake vizuri na ameijengea nchi yetu heshima kubwa sana kitaifa na kimataifa kuhusu uimara wa demokrasia ya vyama vya siasa ndaniya nchi.
 Lakini niseme jambo,hao hao mnaosikia wanalalamika kuhusu msajili wa vyama vya siasa,ukiwapa wao waendeshe nyumba hii ya siasa hawawezi,yaani chama/vyama chao chenyewe kimewashinda ndio wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Chama kinajipambanua kuwa nichakidemokrasia,lakini vita ya madaraka haziishi,Mwenyekiti na timu yake ya uongozi hakuna maelewano.Katibu na naibu wake ni kama paka na panya.Chama kuanzia matendo yake na uongozi wake ni NGO au SACCOS kama sio familia.

Sasa kama yakwao yamewashinda kiasi hiki cha kutisha,wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Mzee J.Tendwa amevilea vyama hivi vizuri sana licha ya uchanga wao kwenye ulimwengu wa siasa za vyama vingi. Biblia inasema usimnyime mtoto mapigo kwasababu atakufa.Hivyo hekima na busara za msajili wa vyama vya siasa aliyestaafu ndio imetufikisha hapa(vyama vya siasa) tunajivunia uwepo wetu katika ulimwengu wa siasa. Unajua hakuna jambo baya na hatari kama kujiona wewe ni bora kuliko mwingine,yaani mawazo yako ndio kila kitu.

Ukifanya jambo wewe na kuliongelea ndio lipo sahihi zaidi kuliko la mwingine, Ni hatari kuona watu wanatoka kwenye ramani kabisa ya siasa,baada ya kuwa wapinzani wa kisiasa sasa ni wapinzani wanchi.
 Naamini amefanya kazi nzuri sana mzee wetu,wale wanaolalamika tunajua ndio tabia yao bila kulalamika hawaishi.Lakini itakuwa safi sana kama watajitazama wao kwanza ndipo wanyoshe kidole kwa mwingine. 

Pia naomba wasije wakawa kama wale wa misri,walitumia nguvu sana kuiondoa serikali iliyokuwepo madarakani,wakaiweka serikali waliyokuwa wanataka,hata miezi sita haijaisha wanatumia nguvu kubwa zaidi kuiondoa serikali waliyoiweka wao wenyewe. Yaani haielweki nini wanakitaka? Mwisho wa siku ni vurugu na malumbano yasiyoa na tija.
 

UNAZUNGUMZIAJE KUHUSU MSAJILI MPYA ALIYETEULIWA WA VYAMA VYA SIASA HAPA NCHINI (MUTUNGI).
 

Mh.Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema
“Niimani yangu kuwa Rais amefanya uteuzi sahahi kabisa,ameona mbali na amemuamini kuwa ataendesha nyumba ya siasa vyema kabisa.Nategemea na niombi kuwa awe mlezi wa vyama vya siasa,akishikiria sharia sana basi ipo siku nchi hii itabakia na chama kimoja tu CCM kwasababu vyama vingi havifuati misingi ya demokrasia,vinajiendesha kama SACCOS.
 Tunaamini katika uongozi wake ataendana na katiba ya nchi kuhusu vyama vya siasa,hasa hii katiba mpya tunayoipigania.Tunaamini ataendeleza ujenzi wa demokrasia safi,siasa za sera na sio siasa za MISITUNI. Unazungumziaje kuhusu nane nane.Mh.Mwigulu Nchemba amesema|”Nawatakia nane nane njema watanzania wote,wakulima watumie nafasi hiyo kujifunza njia mpya za uzalishaji bora,fusa za masoko nan chi iendelee kuneemeka na kilimo. Pia nawatakia waislamu wote kumaliza salama mfungo wa Ramadhani,tudumishe amani na upendo sisi sote ni ndugu,hakuna wa kututenganisha.Tuendelee kuliombea amani Taifa letu,tuwapuuze wote wanaojitahidi kuleta kauli za uchochezi,utengano na uvunjifu wa amani. 

Asante.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...