Saturday, May 24, 2014

JAMAA PANDE ZA IPOGOLO -IRINGA,KAPOTEZA UHAI BAADA YA KUZIDISHA POMBE,



MBALI ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, ‘janki’ Geoffrey Mlelwa (26), mkazi wa Ipogolo mjini hapa, amejikuta akiyakatisha maisha yake kwa kudaiwa kugida pombe kupindukia.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo kijana huyo alikuwa katika Soko Kuu la Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake wakipiga ulabu kwa staili ya kuchanganya (kuchoma sindano) ndipo Geoffrey alipopitiliza na kusababisha apoteze uhai.

NI INDIRECT FIGHT KATI YA CCM NA CHADEMA IRINGA LEO.



MAWAZIRI watatu wako mkoani Iringa na leo Mei 24 wanatarajia kushiriki kikao nyeti kinachohusu mustakabali wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi yaendayo mikoani katika eneo la Igumbilo.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Mazingira Dk Benelith Mahenge na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

Maamuzi yatakayotolewa katika kikao hicho kitakachofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Iringa yatatoa majibu ambayo kwa namna moja au nyingine yataupa ushindi upande fulani wa siasa.

Thursday, May 22, 2014

MSOLA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA KKKT NDENGISIVILI


MBUNGE jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla ametoa Sh 150,000 kama mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Ndengisivili, wilayani Kilolo.
Wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa kanisa hilo, waumini zaidi ya 120 wa usharika huo wanaabudu katika jengo la muda lililojengwa kwa tope huku likiwa limeezekwa kwa nyasi.

Saturday, May 10, 2014

MASANJA AWACHEFUA WAUMINI,,NI BAADA YA KUONEKANA AKICHATI WAKATI WA IBADA.


MSANII mahiri wa komedi ambaye pia ni Mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ amenaswa akichati kwenye simu wakati viongozi wa dini wakishusha maombi mazito.
Tukio hilo lililowachefua baadhi ya waumini lilitokea hivi karibuni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Saba Saba, mjini Moro ambapo Masanja aliyekuwa meza kuu, wakati wenzake wakiongoza sala ya kufungua kongamano hilo, yeye alikuwa bize na simu.
Kitendo hicho kilidumu kwa dakika kadhaa kisha staa huyo ambaye pia ana ndoto ya kuwa mchungaji mkubwa nchini, akajiunga na wachungaji wengine waliokuwa meza kuu kuendelea na sala.

AUDIO-DARASA-SIO MBAYA

Friday, May 9, 2014

VIDEO-P SQUARE-TEST MONEY


KIONGOZI MKUU WA UPINZANI BUNGENI, MH FREEMAN MBOWE ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI VIVULI.




WAZIRI MKUUKIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB)
MIZENGO KAYANZA PETER PINDAFREEMAN AIKAELI MBOWE
WIZARAWAZIRI WA CCMNAIBU WAZIRI CCMWAZIRI KIVULINAIBU WAZIRI KIVULI
(UKAWA)(UKAWA)
1OFISI YA RAISCAPT. GEORGEPROF. KULIKOYELA
(UTAWALA BORA)MKUCHIKAKAHIGI(CHADEMA)
2OFISI YA RAIS
(MENEJIMENTI YACELINA KOMBANIVINCENT NYERERE
UTUMISHI WA(CHADEMA)
UMMA)

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...