Friday, April 18, 2014

CHADEMA,CUF ,NCCR KUUNGANA NA KUUNDA BARAZA LA MAWAZIRI VIVULI BUNGENI


Tumekuwa na mazungumzo na wenzetu na hili jambo ni moja ya mambo ambayo tumekubaliana kushirikiana,
maana kila upande unahitaji mwenzake katika kuikomboa nchi hii” Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Chadema( katikati)

Thursday, April 17, 2014

HATUTARUDI BUNGENI NG'O!!!!!!!NI KAULI YA UKAWA,,WAJIPANGA KUSAMBAZA CD ZA HOTUBA YA LUKUVI KANISANI NCHI NZIMA.


WAJUMBE  wa Bunge Maalumu, wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema hawatarudi bungeni na badala yake kuanzia kesho wataanza mikutano ya hadhara nchi nzima kuwaeleza wananchi juu ya hila za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na washirika wake kutaka kuhodhi mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.
UKAWA wamesema katika mikutano hiyo watazisambaza ‘CD’ zinazomuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akiwa katika Kanisa la Methodist, mkoani Dodoma akiwaeleza waumini wakatae muundo wa serikali tatu.
Walisema kwenye CD hizo, Lukuvi, anaonekana akiwaambia wananchi iwapo wataridhia muundo wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi na Zanzibar itaingia katika utawala wa Kiislamu.

UKAWA WATOA RATIBA YA MAANDAMANO YA KUPINGA MWENENDO WA MCHAKATO WA KATIBA PMYA.


RATIBA YA MAANDAMANO YA UKAWA YENYE LENGO LA KUPINGA MWENENDO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA.
Maandamano ARUSHA,
yataongozwa, na JOHN
MNYIKA, DAR ES SALAAM
yataongozwa na GODBLESS
LEMA NA SUGU, MWANZA
yataongozwa na TUNDU
LISSU NA Prof LIPUMBA,
KILIMANJARO MOSHI
maandamano yataongozwa
na KABWE ZITTO NA CHIKU
ABAO.
MBEYA yataongozwa na
MAALIMU SEFU,
Maandamano ya IRINGA
yataongozwa na SHIBUDA
NA
NASSARI, Maandamano ya
SHINYANGA yataongozwa na
WENJE NA
SALASINI ,Maandamano ya
PEMBA yataongozwa na
MBOWE NA ANNA
KOMU,maandamano ya
TANGA yataongozwa na
HALIMA MDEE NA
MACHEMLI .

TAZAMA LIST YA WASANII WA HIP HOP WENYE MKWANJA MREFU ZAIDI DUNIAN KOTE.

katika list ya wasanii wa hiphop wenye mkwanja mrefu 2014 iliyotolewa na Forbes mtu mzima Diddy ameshika nafasi ya kwanza.
Puff Daddy ameshika nafasi hiyo ya juu katika wasanii wa hiphop bora watano wenye mkwanja mrefu katika list ya forbes iliyoachiwa mapema siku ya jana (April 6). Diddy  ambae pia anajulikana kama Sean "Diddy" Combs ana thamani ya dolla milioni 700, kutokana na kilichoandikwa na gazeti hilo.
Revolt Tv ambayo aliizindua miezi michache iliyopita inamuingizia mkate mkubwa kiasi kwamba kwa siku moja inaweza kumfanya kuwa msanii bilionea wa kwanza wa hiphop, story hiyo iliendelea kusema.

WIMBO RASMI WA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014,


Wimbo rasmi wa kombe la dunia mwaka huu umeshatoka na safari hii Pit Bull Jenifer Lopez na Claudia Leitte ndio wamekula shavu la kurecord wimbo huo.
Wimbo huo umeimbwa kwa lugha tatu ambazo ni Kingereza, Kireno na ki-spanis.

Licha ya kufikisha wasikilizaji 9,223,850 mpaka hivi sasa, asilimia kubwa wauponda wimbo huo, hasa kwa madai ya kuwa pitbull hakufaa kuwepo katika wimbo huo na hata wengine kuuliza inakuwaje wimbo wa kombe la dunia pitubull achane?...




WANAFUNZI WA IFM WAKAMATWA NA BANGI KILO 50.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...