Thursday, April 17, 2014

WANAFUNZI WA IFM WAKAMATWA NA BANGI KILO 50.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa



Basi la New Force lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma.
 Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value).

Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stendi Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma. 

Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bhangi katika mabegi baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam. 


Watu hao walifahamika kwa majina ya:-
1.          CALVIN S/O PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs.
2.          JOHN S/O JOSEPH, Miaka 31, kabila Msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
3.          JOSEPH S/O CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila Msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga. alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs
Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi.





No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...