Thursday, April 17, 2014

TAZAMA LIST YA WASANII WA HIP HOP WENYE MKWANJA MREFU ZAIDI DUNIAN KOTE.

katika list ya wasanii wa hiphop wenye mkwanja mrefu 2014 iliyotolewa na Forbes mtu mzima Diddy ameshika nafasi ya kwanza.
Puff Daddy ameshika nafasi hiyo ya juu katika wasanii wa hiphop bora watano wenye mkwanja mrefu katika list ya forbes iliyoachiwa mapema siku ya jana (April 6). Diddy  ambae pia anajulikana kama Sean "Diddy" Combs ana thamani ya dolla milioni 700, kutokana na kilichoandikwa na gazeti hilo.
Revolt Tv ambayo aliizindua miezi michache iliyopita inamuingizia mkate mkubwa kiasi kwamba kwa siku moja inaweza kumfanya kuwa msanii bilionea wa kwanza wa hiphop, story hiyo iliendelea kusema.



Dr Dre amekamata nafasi ya 2 katika list hiyo, Andre Young ambae ni Rapper na Producer mkwanja mwingi aliotakwa kuwa nao ambao ni dolla milioni 550 zinatokana na mzigo wa headphones "Beats by Dre" kampuni ya headphone ambayo alianzisha na Jimmy Lovin  2008

Jay Z ametua katika nafasi ya 3. dili lake na Rocawear pamoja na Live Nation imemuingizia dolla milioni 150, iliyomsaidia kuongezea na kufika kukusanya dola milioni 520 

 Brian "Birdman" Williams ambae pia anajulikana kama Baby, ameingia katika nafasi ya 4 ya list ya Forbes, asilimia zake 50 kutoka Cash Money Records inamuingizia zaidi katika mkwanja wake ambao ni dola milioni 160

 Na wa tano ni Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ambae utajiri wake mkubwa unatokana na maji yake ambayo ameyaita Vitamin Water ambayo yamemsababishia kupata kile kilichoripotiwa kuwa ni dola milioni 100


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...