Tanzania
bado ipo kwenye mgogoro na nchi ya Malawi juu ya mpaka halisi wa nchi,Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Benard Membe amesema hatma juu ya
mgogoro huo inategemewa kutolewa mwezi march.
Hukumu hiyo itaamuliwa
baada ya jopo la Usuluhishi litakapokaa na kusikiliza pande zote mbili ambalo
litaongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano
Kupatikana kwa suluhu ya
mgogoro wa mpaka huo kutawatoa hofu wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa hilo
ambao wamekuwa wakitegemea shughuli za uvuvi wakiwemo wakazi wa kijiji cha
Manda Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Wakazi wa eneo hilo
wamesema kwa hivi karibuni tangu kutulia kwa vuguvugu la mgogoro huo wamekuwa
wakiendelea shughuli zao za maendeleo kama kawaida ikiwemo uvuvi.
No comments:
Post a Comment