Saturday, February 22, 2014

KUMEKUCHA KALENGA,KAMPENI ZA KUWANIA UBINGE WA JIMBO HILO KUZINDULIWA LEO KWA UPANDE WA CHADEMA,HUKU CCM WAKIJIPANGA KUZINDUA KESHO.


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa leo Jumamosi atazindua kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa katika kijiji cha Kalenga.

Kwa upande wao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitanzaa kampeni zake keshokutwa Jumapili katika kijiji cha Mseke wakati kikiendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hizo.


Uchaguzi huo unakishirikisha chama kingine cha Chausta kilichomsimamisha Richard Minja kupeperusa bendera yake.
CCM kwa upande wao imemsimamisha, Godfrey Mgimwa, huku Chadema ikiwa imemsimamisha Grace Tendega.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka, jimbo la Kalenga lina jumla wapiga kura 85,051.

Akizungumza na www.frankleonard.blogspot.com Katibu wa Chadema Iringa Vijijini, Felix Nyondo alisema Dk Slaa atawasilia mjini Iringa kwa gari mapema kesho katika mapokezi yatakayohusisha msafara mkubwa wa magari na pikipiki katika eneo la Ndiuka mjini hapa.

Mbali na Dk Slaa, Nyondo alisema wengine watakaokuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni hizo ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Leman na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Alisema baada ya uzinduzi huo, Chadema itaendelea na kampeni za kila siku na kwa mujibu wa ratiba yao, kila siku watakuwa wakifanya mikutano 39.

Nyondo alisema katika kampeni hizo Chadema itatumia helkopta (chopa) tatu, magari 56 na pikipiki 80.

Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitagawanywa katika kata zote 13 za jimbo hilo ili kufanikisha shughuli nzima ya kampeni zao.

Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassana Mtenga alisema CCM kwa upande wake inaendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni zake.




Katika uzinduzi huo ambao hata hivyo hakutaja tarehe yake, alisema viongozi mbalimbali wa CCM ngazi ya Taifa, Mkoa na wilaya watashiriki.

“Kabla ya uzinduzi huo tutakuwa mikutano kadhaa, mikutano hiyo tunaiita ya rasharasha kabla shughuli nzito haijaanza; kwa kuanzia tutafanya mkutano wetu wa kwanza katika kijiji cha Mseke, Jumapili keshokutwa,” alisema.


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...