Wednesday, July 31, 2013

IELEWE HIP HOP,,,,,

Vijana wengi sana tunapenda mziki wenye mahadhi ya kufokafoka,,yaani Hip hop,,lakini wengi wetu  hatujui historia ya mziki huo,,,leo kwenye sesction hii 'KUTOKA CHIMBO" tutajaribu kuangazia historia ya mziki huu unaopendwa na wengi..

CHEKI NA HII!!!!

Hip hop ni aina ya muziki unaoelezea aina ya usanii na utamaduni fulani uliyotokana na jamii ya Wamarekani Weusi na Walatino kunako miaka ya 1970 huko mjini New York City, hasa katika kitongoji cha Bronx.[1][2][3] DJ Afrika Bambaataa alieleza kwa muhtasari wa nguzo nne za utamaduni wa hip hop: U-MC, U-DJ, breaking na uandikaji wa graffiti.[4][5][6][7] Elementi zingine ni pamoja na beatboxing.[8]Kwa vile imeibukia kutoka mjini South Bronx, utamaduni wa hip hop umeenea dunia nzima.[9] Muziki wa hip hop awali ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa wanatengeneza midundo kwa kutumia mtindo wa kurudirudia na kusimama (hasa katika visehemu vidogo vya muziki wa kusisitiza mwelekeo wa kigongoma) kwenye turntable mbili, hasa hujulikana kama kusampo muziki.
Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16 katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.
                                                             

Muundo kamili wa kudansi na staili kadha wa kadha za mavazi zimezua mashabiki miongoni mwao katika muziki mpya. Elementi hizi zimeonesha mabadiliko ya na maendeleo kadha wa kadha katika historia ya utamaduni huu. Baadhi ya miziki ya hip-Hop hutoa maelezo ya kisiasa.
Mahusiano baina ya graffiti na utamaduni wa hip hop unatokana mionekano mipya tofauti iliyoongeza ufafanuzi wa kina na uenezi tofauti wa kivitendo ambapo kwingine walichukulia elementi ya hip hop kama sehemu ya sanaa, kukiwa na mpitilizo mkubwa baina ya hao wanaondika graffiti na hao wanaotenda elementi zingine za hip hop kivyao. Leo hii, graffiti imebakiwa kuwa sehemu ya hip hop, wakati kwa upande wa sanaa imechukua eneo kubwa katika masuala ya picha na michoro katika maeneosho mbalimbali duniani kote.

NEXT TIME TUTAANGALIA KIUNDANI NGUZO ZA HIP HOP!!!!

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...