Thursday, February 13, 2014

PATA KUJIKUMBUSHA,KUELEWA KWA UFUPI NINI MAANA YA 'VALENTINE DAY',


Hii ni vizuri kuifahamu  wakati unasherehekea siku hii ya Valentine na yule umpendaye ni vizuri kujua maana halisi ya hii Valentine Day ambayo imeapishwa kufanyika kila mwaka February 14.
Neno Valentine lilitokana na jina ‘Valentino’ huyu alikuwa Mtakatifu wa Kiroma aliyeitwa Valentino,siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya wapendanao na wengi wanaiita ‘Valentine Day’ ni maadhimisho ambayo hufanyika kila  mwaka.

Watu wengi husherehekea siku hii kwa kuonyesha upendo,kuthaminiana pamoja na kujaliana kati ya watu wenye mahusiano mbalimbali ya karibu japo mara nyingi siku hii hutumiwa na walio kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Valentine Day,asili ya  Siku hii ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwa ajili ya kuupenda Ukristo na Kihistoria Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia.
Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga,Mtakatifu Valentino aliteswa kwa ajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa  February 14 Kwa ajili ya msimamo,imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza February 14 kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.Happy Valentine Day

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...