Tuesday, August 27, 2013

VYUO VIKUU VYA LIBERIA KUKOSA WANACHUAO BAADA YA WANAFUNZI WOTE WA FORM SIX KUFELI MITIHANI YAO.

Inakuaje pale wanafunzi wa form six ambao wanatarajiwa kujiunga na chuo kikuu wanafeli wote nchi nzima na kushindwa kujiunga na chuo kikuu?.Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Chuo kikuu cha Liberia kwa mwaka 2013/2014 hakitakuwa na mwanafunzi hata mmoja kwa ajili ya kozi yoyote ile kutokana na wanafunzi hao kufeli. Waziri wa elimu wa Liberia anasema wanafunzi wameshindwa kufaulu mtihani huo kutokana na lugha walioitumia ya kiingereza. Wanafunzi hao hawakuwa na uelewa mzuri wa lugha ya kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Hata hivyo wanafunzi wengi hawana imani na matokeo hayo na waziri wa elimu anajaribu kuongea na chuo kikuu cha Liberia kuona jinsi watakavyofanya.



No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...