Monday, August 5, 2013

RAPPER 50 CENTS AKUMBANA NA BALAA LINGINE.

50 CENTS



Rapa na muigizaji 50 Cent  anakabiliwa na mashtaka ya  kumshambulia girfriend wake wa zamani .

Kesi hiyo ya rapper na mwigizaji, ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, ilikuwa imepangwa kusikilizwa Jumatatu.yaani leo!! 

Kama atapatikana na hatia the hit maker wa "In Da Club" atakabliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela na faini ya $ 46,000  . 

Mwanamke huyo  aliwaambia polisi kwamba  Juni 23, Jackson alianza kuharibu vitu vyake vya ndani kabla ya yeye kujifungia chumbani. 
Anasema Jackson alipiga mateke mlango akimlazimisha kufungua na hivyo kumsababishia  kuumia. 

Polisi wanakadiria kutokea uharibifu wa hadi   $ 7,100 katika nyumba hiyo. 

mwanamke huyo  aliwaambia polisi kuwa yeye alikuwa katika uhusiano wa miaka mitatu na ana mtoto na Jackson ambaye anahusishwa na  kushughulika na biashsara za madawa ya kulevya na vurugu katika nyimbo zake  nyingi.



No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...