Tuesday, August 6, 2013

HATUWEZI KUACHIA DOLA 2015- NI KAULI YA JANUARY MAKAMBA MBUNGE WA BUMBULI -CCM

MH.Janiary Makamba

MJUMBE wa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. January Makamba, amesema chama hicho hakiwezi kuanguka katika Uchaguzi Mkuu 2015 na wanaosema kimefikia ukingoni kuongoza dola wamepotea.
Bw. Kamanda aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Tanga uliofanyika katika ukumbi wa Mamba Club mjini Korogwe.

“Kuna maneno yanasemwa mitaani kwa bahati mbaya hata baadhi ya wana CCM wenzetu wanaogopa na wanayaamini kuwa ya kweli lakini mimi nimekuja kama mjumbe, nataka kuwapa siri ya Kamati Kuu, kamwe CCM haiwezi kuachia dola mwaka 2015.



“Hali ya unyonge kuwa tutashindwa mwaka 2015 imepandikizwa, wapo wanaosema CCM inakimbiwa na vijana lakini ukiangalia mkutano huu hakuna chama kinachoweza kuwakusanya vijana kama hivi zaidi yetu,” alisema.

Alisema moja ya mikakati ya kuifanya CCM isiondolewe madarakani ni vijana kuisemea mahali popote ambapo vyama vya upinzani vinaonekana kuungwa mkono na vijanakwa sababu ya mikutano mingi waliyoifanya.

Naye Bw. Yusuph Makamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, alitumia fursa hiyo kutangaza kujiuzulu nafasi ya Kamanda wa UVCCM, mkoani hapa na kutaka uchaguzi huo utumike kuwaweka viongozi wenye mvuto ili chama hicho kiweze kuibuka na ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu 2015.

“Ili mchezaji aonekana mzuri lazima awe na pumzi ya kucheza dakika 90, lakini kama hana uwezo huo msimpe nafasi hiyo na kama anacheza lakini anaonekana kuchoka, lazima apumzishwe na kupewa nafasi yake mtu mwingine,” alisema Bw. Kamamba.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa ambaye alimaliza muda wake, Bw. Rodgers Shemwelekwa, aliwataka vijana waache kuchagua wagombea wanaotoa rushwa ili wachaguliwe.

“Msikubali kupewa fedha na wagombea ili wawatumie kama ngazi ya kupata madaraka ya uongozi,” alisema.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...