Saturday, August 31, 2013

BAADHI YA MAONI YA CHADEMA KUHUSU KATIBA MPYA.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeeleza kuiunga mkono rasimu hiyo kwa asilimia 80 kulingana na maoni ya watu milioni 3.4 waliokusanya.Hata hivyo, CHADEMA imeainisha hoja 11 ambazo wananchi wamependekeza ziongezwe katika rasimu hiyo ya Katiba mpya.Akizungumza na waaandishi wa habari jana makao makuu ya chama hicho, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema mrejesho huo umepatikana baada ya kuwazungukia wanachama wao na Watanzania wengine kwa wiki mbili.Dk. Slaa alisema maoni hayo yamekusanywa kupitia kanda 10 za chama hicho na Watanzania waishio nje ya nchi kwa njia ya kisayansi huku yakiwa na vithibitisho tofauti na vyama vingine vya kisiasa.

TETESI,,,MWANAHAKATI WA CCM BW MOHAMED RIAMI (EDDY RIAMI) ATANGAZA KUJITOA RASIMI CCM

Mwanaharakati Maarufu Bw Mohamed Riami (Eddy Riami) ametangaza kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Kongamano lililotayarishwa na Kamati ya Maridhiano, hii ilikuwa strong speech iliyowahi kutolewa na Bw Eddy Riami amesema yeye sio mwanasiasa, akiwafananisha na Jusa na Mzee Moyo. Bali yeye ni raia kama walivyo raia wengine.

Amewataka Wazanzibar kujitolea kutafuta heshma zao na nchi yao.

Alisema kwamba ni wao ndio waliompigia kura Rais kwani Rais mwenyewe hakupiga kura katika uchaguzi uliopita. Hivyo anajuwa vipi Zanzibar itashinda kabla ya mwaka 2015. Alikuwa akikariri moja ya hotuba ya Mzee Karume alpokuwa anakadiria kuwa Zanzibar haihitaji uchaguzi
hadi baada ya miaka 50.

Ametaka suala la siasa litolewa katika katiba mpya. Vilevile amewataka viongozi wengine kuachana na siasa badala yake kupigania Zanzibar nje ya siasa. Kwani ni siasa ndio iliyoifikisha hapa Zanzibar.

JAY JAY OKOCHA,,NGULI WA SOKA ALIYEMAUA KUANZA KUFANYA FILAMU..

Majek Fashek, Jay Jay Okocha

Augustine Jay Jay Okocha, Mwanasoka kutoka Nigera ambaye amejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kucheza soka kitaifa na kimataifa, aameamua kubadilisha fani baada ya kuwa katika soka kwa miaka mingi sasa.

WABUNGE WATAKA MBIO ZA MWENGE ZIFUTWE,

MBIO za Mwenge wa Uhuru nusura ziahirishe shughuli za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kutaka zifutwe na hoja hiyo ijadiliwe bungeni.
  
Hata hivyo, suala hilo liligeuka shubiri kwa Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kuzomewa na kurushiwa maneno ya kejeli alipojaribu kuzitetea mbio hizo.
  
Chanzo cha mzozo huo kilitokana na maswali ya mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), aliyeihoji serikali kama kuna uwezekano wa kutoukimbiza Mwenge katika maeneo ya watu wasiouhitaji.

DIAMOND NA LINAH LIVEEE!!!!

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
  

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.

TAZAMA PICHA 10 WAKATI WA UZINDUZI WA FILAMU YA LULUI.

Thursday, August 29, 2013

MAKINDA APIGIWA DEBE KUGOMBEA URAISI 2015


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, amempigia debe Spika wa Bunge, Anne Makinda, akisema kuwa anafaa kuwa rais kutokana na sifa zake.

Profesa Mwandosya alimwaga sifa hizo bungeni jana, wakati akiunga mkono Azimio la Bunge la kumpongeza Makinda, kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA).

MEJA JENERALI WA JESHI LA TANZANIA (JWTZ) AUAWA NA MAJESHII YA M23 HUKO KONGO.



KINSHASA, Congo (AP) — United Nations forces and the Congolese army attacked rebel positions with helicopter gunships, armored personnel carriers and a phalanx of ground troops Wednesday, ramping up the U.N.'s engagement in the latest rebellion to roil this country's tormented east.

MAJAMBAZI WALOVALIA SARE ZA POLISI WAPORA BENKI YA HABIB ILIYOPO KARIAKOO.

Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha.


 Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo..

Habari  zaidi  baadae. 


MWIGULU NCHEMBA ATAKA MBOWE NA DR.SLAA WAKAMATWE KWA MAUAJI YA RAIA.

MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), amechafua hali ya hewa bungeni kwa kuitaka Serikali kuwachukuliwa hatua viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge huyo alisema mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa madai ya kusababisha mauaji ya raia. 

ANGALIA PICHA NNE ZA BINADAMU MWENZETU HUYU.

Wednesday, August 28, 2013

KING CRAZY GK IZ BACKKKK!!!!KUWA WA KWANZA KUSIKILIZA NA DOWNLOAD NGOMA HIII HAPA,,BARAKA AU LAAN NDO JINA LAWIMBO,

 Baada ya ukimya wa miaka sita bila ngoma wala interview, leo King Crazy GK akiwa amesindikizwa na East Coast Team nzima kuanzaia AY, Mwana FA, Buf G (Gizinga), Paulin Zongo, Yuzo pamoja na Snea, ameibuka na kudondosha single mpya "Baraka au Laana"  aliyomshirikisha Yuzo Baraka au laana ni swali ambalo nimewaachai watanzania wajiulize, ni baraka au ni laana uzaliwa Afrika, unajua kitaka kujua kile anachokiwaza mwingine muulize swali, akianza kufunguka ndio utajua anawaza nini juu ya ulichomuuliza, so hili ni swali kwa Watanzania. tumekuwa tukiskia watu wakisema bora kuzaliwa paka Ulaya kuliko kuzaliwa binaadam Afrika, kwasababu kule wanyama wanatimiziwa haki zao kuliko sisi huku, sasa tujiulize is it true..amesema GK."


DYANA NYANGE AMTUHUMU DIAMONDI KWA KUMUIBIA WIMBO WAKE,,



Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha, nataka kulewa. Msanii  Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma baada ya kusadikiwa wimbo anaotaka kuuachia wa No.1 ni wa Dayna. Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna.
hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia. skiliza na pia waweza ku share na wenzio
                                                     msikilize dyna hapa


SHILOLE ACHEZA NUSU UCHI KWENYE TAMASHA LA FIESTA,,ANGALIA PICHA HIZI..



















Tuesday, August 27, 2013

WENGI SANA ESPECIALLY HAPA TZ HUWA TUNAFIKIRI KWAMBA KWA UMAARUFU WA GARI KAMA RANGE ROVER NA VX,HUENDA HIZI GARI NDO ZITAKUA NDO THE MOST EXPENSIVE DUNIANI,,MAMBO NI TOFAUTI HEBU ANGALIA TOP TEN YA GARI ZA BEI ZAIDI DUNIANI -2013

1 Bugatti Veyron Super Sports $2,400,000

This is by far the most expensive street legal production car available on the market today (the base Veyron costs $1,700,000). Capable of reaching 0-60 mph in 2.5 seconds, the Veyron is the fastest street legal car when tested again on July 10, 2010 with the 2010 Super Sport Version reaching a top speed of 267 mph (430 km/h). When competing against a Bugatti Veyron, you better be prepared!
2 Aston Martin One-77 $1,850,000

FAT JOE KUTUPWA LUPANGO MIEZI MINNE KWA KOSA LA KUKWEPA KULIPA KODI.

the hit maker wa whats love,, aloha na ngoma  kali nyingi sana FAT JOE  43, jana ameenda kuanza maisha yake kama mfungwa kwa kosa la kukwepa kulipa kodi,
Kabla ya kuenda kuanza kifunga chake fat joe alitweet na kuwaambia mashabiki wake kwamba wasiwe na wasi kwani atarudi mara tu baada ya kumaliza muda wake gerezani.
fat joe amehukumiwa kifungo hicho kwa kosa la kukwepa kodi kiasi cha dola miliani 30 hapo mwaka 2007 na 2010.

PICHA,,RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI FRANSIS MUTUNGI NA NDUGU JOHN TENDWA ALIYEACHIA MADARAKA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Jaji Francis Mutungi na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Mhe John Tendwa baada ya kumuapisha Jaji Mutungi Ikulu jijini Dar es Salaam .


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinakubaliana na rasimu ya Katiba kwa sababu asilimia 80 ya rasimu hiyo kwa kile inachoeleza inalinda maslahi ya wananchi.Kadhalika Chama hicho kimependekeza kuingizwa kwa kipengele cha haki ya wakulima na wafugaji katika Katiba mpya huku, kikiunga mkono kuwapo kwa serikali tatu .

KAIMU MKURUGENZI WA WILAYA YA KILOLO NGUGU BENSON KILANGA APATA AJALI MJINI IRINGA

hilindo gal ya kaimu mkurugenzi lililonusurika ajali.

UNYAMA-KIJANA ACHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA GUNIA LA MKAA HUKO MBAGALA-TEMEKE


NEY WA MITEFO NA CHID BENZI WAMALIZA BIFU LAO,,MADEE NDIYE ALIYEWAPATANISHA,


Yeyote ambae damu yake ipo sana kwenye muziki wa bongofleva ni lazima atakua anafahamu kuhusu ugomvi wa muda mrefu, kutoelewana kwa Chidi Benz na Ney wa Mitego, ishu ambayo ilihusishwa hata kwenye nyimbo zao.
Shuhuda mkuu wa tukio lenyewe ni msanii Madee ambae naanza kwa kumkariri anasema ‘hizi ndio faida za Serengeti Fiesta, kujuana na kukutana na watu wengi, hiki ni kitu ambacho nilikipanga mimi… watu wanafikiria tu sisi tunakwenda kule kufanya muziki, mbali na pesa tunazolipwa vizuri sasa hivi kwenye Fiesta, kuna faida nyingine pia, niliposikia Chidi Benz yupo kwenye Fiesta nilijipanga lazima nifanye hivi manake Chidi na Ney wote nawajua, nimekaa nao’

VYUO VIKUU VYA LIBERIA KUKOSA WANACHUAO BAADA YA WANAFUNZI WOTE WA FORM SIX KUFELI MITIHANI YAO.

Inakuaje pale wanafunzi wa form six ambao wanatarajiwa kujiunga na chuo kikuu wanafeli wote nchi nzima na kushindwa kujiunga na chuo kikuu?.Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Chuo kikuu cha Liberia kwa mwaka 2013/2014 hakitakuwa na mwanafunzi hata mmoja kwa ajili ya kozi yoyote ile kutokana na wanafunzi hao kufeli. Waziri wa elimu wa Liberia anasema wanafunzi wameshindwa kufaulu mtihani huo kutokana na lugha walioitumia ya kiingereza. Wanafunzi hao hawakuwa na uelewa mzuri wa lugha ya kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Hata hivyo wanafunzi wengi hawana imani na matokeo hayo na waziri wa elimu anajaribu kuongea na chuo kikuu cha Liberia kuona jinsi watakavyofanya.



ZITTO KUTOGOMBEA URAIS 2015

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

TAZAMA SEHEMU YA MECHI KATI YA MAN U NA CHELSEA ILIYOCHEZWA JANA,


Monday, August 26, 2013

NOMA SANA WADAU,,HII NI KWENYE MTV AWARDS SIKU YA JANA.


MTV AWARDS,,!!!!


AFRICA TUNARUDISHWA KWENYE UKOLONI...!!??SOMA,TAFAKARI,,,CHUKUA HATUA,,,


HAYA ninayoyaandika leo katika safu hii yanaweza kuwa si mageni. Inawezekana kabisa ni marudio ya kilichokwishakuandikwa.
Huenda pia ni mambo yanayoudhi baadhi ya watu ama kwa maudhui yake au kwa kurudiwarudiwa kwake. Mara nyingi kuhoji mazoea si jambo linalopokewa vyema hasa na wale wasioona tatizo katika hali ilivyo (status quo).
Leo ninapenda kudadisi kwa ukaribu zaidi hicho ninachokiona huko tunakoelekea kama jamii ambako huenda si wengi wetu wanaoona umuhimu wa kufanya hivyo. Kabla sijaingia katika udadisi huo nirejee kwa kifupi utangulizi wangu ambao utaweka mawazo yangu ya leo katika muktadha wake kamili.

NIKK MBISHI NI MUATHIRIKA WA UKIMWI!!!!??


Tumekuwa  tukishuhudiwa  vituko  mbalimbali  vya  wasanii wetu  ambao  wamekuwa  wakihangaika  usiku  na  mchana  kuusaka  umaarufu....

Wapo  ambao  wamekuwa  wakivua  nguo  zao  jukwaani, wapo  ambao  wamekuwa  wakipiga  picha  za  uchi  na  kuzitupia  mitandaoni.Yote  hiyo  ni  kutafuta  Jina  au  umaarufu ambao  mimi  binafsi  nauita  ni  umaarufu  wa  kishamba.....

ANGALIA VIDEO MPYA YA YOUNG DEE,,-KIJUKUU,


DADA WA MBOWE ATIMKIA CCM.


DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

TAZAMA PICHA 10 ZA KWENYE RED CARPET WAKATI WA MTV MUSIC AWARDS.


DILLISH KUTOKA NAMIBIA AIBUKA NA MADORALI YA BBA.



Mshiriki kutoka Naibia "Dillish" ndio mshindi wa Big Brother Africa (the chase) alieondoka na dola 300,000 katika fainali zilizofanyika usiku huu (August 25th).
Dillish mwenye miaka 24, hajawahi kuwa head of the house hata siku moja katika siku zote 91 alizokuwa ndani ya jumba, alishawahi kuwa nominated mara 5 na mara zote alibaki kwa kura za Africa, na hajawahi kuwa na mahusiano na mshiriki yoyote.

HATIMAYE FOOLISH AGE YA LULU YARUHUSIWA KUINGIA SOKONI.



Siku chache baada ya kutangaza kuzindua filamu yake mpya "Foolish Age" , lulu ametoa statement inayoonyesha kuwa kumekuwa na maneno ya kuwa filamu hiyi imezuiliwa na bodi ya ukaguzi wa filamu. kupitia acc yake ya Instagram, Lulu amesisitiza kuwa Filamu yake imeshakaguliwa na tayari ameshapata kibali kuendelea na uzinduzi huo.

WACHUNGAJI WAHUSISHWA NA UFREEMASON,,SOMA RIPOTI KAMILI HAPA.



HIZI habari zimekuwa ya kushtua sana kwangu japo mambo kama haya nilitegemea sana kuyaskia leo katika pitapita za mitandaoni nikaliona hii Habari ya wachungaji mafreemason, kwakweli inashtua sana na sasa wakristo na wafuasi wa madhehebu yote inabidi kuwa makini sana na hii hali tusije tukajikuta tunajutia maisha yetu baadae.

Friday, August 23, 2013

ANGALIA WIMBO MPYA WA JOKATE NA LUCC-KAKA NA DADA.



KWA MARA YA KWANZA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WAMUWEKA HADHARANI MTOTO WAKE

Kanye west leo hii kwa mara ya kwanza ameonyesha picha ya mtoto wake na Kim Kardashian " North West" katika kipindi cha television cha Kris Jenner ambae ni mama yake na Kim.
Mwanzoni Kim na Kanye walikuwa na ubishani juu ya kutumia picha ya mtoto wao kupata pesa kwa ajili ya charity, lakini inaonekana Kanye ameona kupitia kipindi cha mama mkwe wake ndio poa..maana ni kipindi kipya labda anataka kumpandishia chati.

SIKILIZA HISTORIA YA DIAMOND,,KUMBE JAMAA ALIKUA MUUZA MITUMBA,,CHEKI VIDEO HII AKIWA TABORA KWENE TAMASHA LA FIESTA.




Hitmaker wa 'Moyo Wangu' Naseeb Abdul akiwa ni miongoni mwa wasanii walio katika ziara ya Serengeti Fiesta sasa leo kwenye semina ya fursa huko mkoani Tabora aliweza kufunguka na kueleza jinsi alivyosota,alivyouza mitumba,mafuta na kazi ya kiwadani.

Itazame hii video hapa uone jinsi akielezea katika Semina ya Fursa mkoani 

FIAMU MPYA YA LULU YA FOOLISH AGE YAZUILIWA KUTOKA,,,SABABU NI MAVAZI YASIYOENDANA NA MAADILI YA KITANZANIA.


Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”

Thursday, August 22, 2013

STAA WA TAMTHILIYA YA "PRISON BREAKER" AJITANGAZA KUWA NI SHOGA.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na mtandao wa the people.com,Wentwoth ameweka wazo  taarifa hiyo kwenye barua aliyo andika kukataa mwaliko kuhudhuria tamasha la filamu la kimataifa la st petersburg nhini urusi
Barua hiyo ilichapishwa kernye mtandao wa “gay lesbian alliance against defamation”

WEMA SEPETU TENA!!!! ANASWA NA JAMAA MWINGINE KABISA.


LICHA ya kunaswa katika matukio tofauti, Wema Sepetu hasikii. Safari hii imenaswa picha inayomuonesha akimshushia busu motomoto jamaa anayefahamika kwa jina la Rommy Jonson.
Picha hiyo ambayo inamuonyesha wema akimbusu jamaa huyo katika pozi lenye hisia kali za kimapenzi imenaswa katika mtandao wa kijamii wa instagram


ALAWITI MTUMISHI NA KUSAMBAZA VIDEO


JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limemkamata mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, Totolii Kimath anayedaiwa kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliliambia Tanzania Daima kuwa kijana huyo ambaye anamiliki maduka ya kuuza na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Dubai.

POLISI FEKI WENGINE WANASWA.


SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari feki wa usalama barabarani, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watuhumiwa saba wa ujambazi, wakiwa na sare za Polisi, huku mwingine akijifanya ofisa Usalama wa Taifa.
  
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na sare za Polisi jozi mbili.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...